Habari/News

Serikali yatangaza ukaguzi wa Magari nchi nzima

Tarehe February 24, 2018

Serikali kupitia kwa  Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza kua kuanzia tarehe 1 Machi 2018 watafanya  ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima.

Kwa mujibu wa Masauni amesema kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.

Amesema Wamiliki wa magari madogo wanatakiwa kupeleka magari yao katika vituo vya polisi ili yafanyiwe Ukaguzi kama yanastahili kuendelea kuwepo barabarani.

Nataka madereva  wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja“Amesema Masauni

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni