Afya

Serikali yatangaza Ajira 6,180,sifa za kujiunga hizi hapa

Tarehe May 11, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo.

Wafanyakazi wapya zaidi ya 6,180 wata ajiriwa Serikalini katika sekta ya afya ili kuweza kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya.

Hayo yamesemwa na  2018 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo na kubainisha kuwa  watumishi hao wataajiliwa kabla ya mwaka kuisha na kuongeza kwamba lengo la serikali ni kuboresha sekta ya afya nchini.,

Watakaoajiriwa ni wenye sifa zifuatazo, Awe raia wa Tanzania, kuambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne na sita, cheti cha taaluma.

Pia asiwe muajiliwa wa serikali au shirika la dini ambapo mshahara wake unalipwa na serikali, umri usizidi miaka 45 na utayali wa kufanyakazi mahali popote nchini

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni