Habari/News

Serikali yatahadharisha TANESCO na vishoka

Tarehe October 12, 2017

Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani.

Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ametangaza kiama kwa watumishi wote wa TANESCO na vishoka watakao bainika kushirikiana na wateja kuiba umeme huku akielezea mikakati yake kuhakikisha umeme unakua wa uhakika.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo alipokuwa akiongea na maafisa wa TANESCO, na kusema shirika limekuwa likipoteza mapato makubwa kufuatia umeme unaopotea, kutokana na kuhujumiwa miundo mbinu yake, na wizi wa umeme uliokithiri unaofanywa na baadhi ya wateja.
Taarifa hiyo imetolewa  baada ya  TANESCO kugundua wateja zaidi ya mia moja wanatumia umeme bila kulipia hali inayolitia hasara shirika, baada ya kufanya operesheni maalum ya kukagua watu wanaoiba umeme jijini Dar es salaam.
Kufuatia operesheni hiyo, baadhi ya watu wamekuwa wakiyakimbia makazi yao kuogopa kutiwa mikononi mwa polisi, na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri Kalemani amesema hayo ikiwa ni siku chache tu tangu kula kiapo cha kuwa Waziri wa Nishati na Madini baada ya Rais, Dkt. John Magufuli kuitenganisha iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini na kuwa wizara mbili zinazojitegemea.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni