Habari/News

Serikali yafuta mafao kwa waliogushi vyeti

Tarehe February 13, 2018

Hatimaye serikali   imetangaza  msimamo wake kwa watumishi wote waliobainika kuwa na vyeti feki na wale wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji, Sera Mathias Kabundugulu amesema watumishi wote waliobainika kuwa na vyeti feki na wale wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne hawana madai yoyote.

Amesema watumishi ambao wamebainika na kuondoka wenyewe, wamefutwa kwenye orodha ya watumishi wa umma na hawana madai wanayodai serikalini ukiwa ndio msimamo wa Serikali kwa sasa.

Kabundugulu amesema pamoja na zoezi kukamilika kwa muda ambao umepangwa, wapo baadhi ya maafisa utumishi wameendelea kuwafumbia macho watu wasio kuwa na vyeti vya kidato cha nne.

Mwaka jana  Serikali iliwaondoa watumishi zaidi ya 9000 waliokutwa na vyeti ‘feki’ katika ukaguzi uliofanyika nchi nzima.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni