Habari/News

Serikali yadai mahusiano na Kenya mazuri ikijiandaa kupiga mnada ng’ombe wengine

Tarehe November 14, 2017

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina.

Serikali imesema kuwa uhusiano wa Tanzania na nchi nyingine washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mzuri na kwamba hakuna ushirikano wa kihalifu.

Hao yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019 Bungeni, Mjini Dodoma kufuatia taarifa za hivi karibuni katika mitandao ya kijamii zikieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Kenya umezorota baada ya kuchomwa kwa vifaranga vya kuku zaidi ya 6,000 na kupigwa mnada wa ng’ombe waliokamatwa kutoka nchini Kenya.

Waziri Mpina amesema walioingiza ng’ombe hao ni wahalifu na wamevunja sheria za nchi ambazo zinaongoza nchi zote hivyo hakuna mtifuano wowote wa kidiplomasia bali ni watu wachache waliovunja sheria.

Ametahadharisha wafugaji wa nchi jirani kufuata sheria wanapotaka kuingiza mifugo nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mpina ametangaza kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 10,000 wa nchi za Uganda na Rwanda waliokamatwa katika operesheni inayoendelea nchini.

Amesema ng’ombe hao watapigwa mnada wakati wowote kama ilivyofanya kwa ng’ombe 1,325 wa Kenya.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni