Habari/News

Serikali yachukua maamuzi magumu kwa aliyesimamia kiapo cha Odinga

Tarehe February 7, 2018

Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna

Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefukuzwa na kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM , kulingana na wakili wake Nelson Havi na Cliff Ombeta.

Bwana Ombeta amesema kuwa aliarifiwa kwamba bwana Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada.

Wakili mwengine Dkt. John Khaminwa alisema kuwa mteja wake tayari ameondoka Kenya.

“Ni kweli .Alilazimishwa kuingia katika ndege ya KLM dakika chache tu kabla ya saa nne usiku na tumebaini kwamba anaelekea Canada. Ni ukiukaji mkubwa wa haki”, alisema Dkt Khaminwa kwa simu.

Haijulikani ni sheria gani iliotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo.

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi baadaye alisema kuwa bwana Miguna alikamatwa baada ya kukiri kumpatia kiapo kiongozi wa Nasa Raila Odinga mbali na kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa marufuku la NRM.

.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni