Habari/News

Serikali kupunguza miaka Elimu ya Msingi,binti kuolewa lazima kidato cha nne

Tarehe November 10, 2017

Serikali imesema inatarajia kuufumua mfumo wa elimu ya msingi ambao ulikua ni miaka saba kumaliza elimu msingi na sasa itakua miaka 6 pekee.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Joseph Kakunda wakati  akitolea ufafanuzi wa watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari.

Amesema mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima.
“Napenda kutoa majibu sahihi waliopata mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu huko tunakoelekea inabadilisha mfuo wa sasa wa elimu ambao utahitaji mtoto aanze chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari miaka minne na itakuwa ni lazima”, amesema Mheshimiwa Kakunda.
Amesema  kupitia mfumo huo baada ya kuhitimu ndio utakuwa kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na ndipo ataruhusiwa kuolewa.
Suala la binti kuolewa mpaka awe na cheti cha kidato cha nne limeonekana kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii,ambapo asilimia kubwa ya watu wakihoji itakuwaje kwa mabinti waliofeli darasa la saba na kushindwa kuendelea kidato cha kwanza.a

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni