Habari/News

‘Scorpion’ atupwa lupango miaka saba

Tarehe January 22, 2018

Mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete .

Mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete maarufu kama  Scorpion leo amehukumiwa kwenda jela  miaka 7  kwa kosa la kumjeruhi na kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho.

Scorpion amehukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo ametakiwa pia kulipa faini ya shilingi milioni 30 kama fidia kwa majeruhi.

Kwa upande wake, mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni majeruhi, Said Mrisho amelia mahakamani hapo akidai adhabu aliyopewa Scorpion haitoshi ikilinganishwa na kosa alilotenda huku akieleza kuwa atakwenda kwa Rais Dkt. John Magufuli kumueleza masikitiko yake.

Katika kesi hiyo  Njwete (Scorpion) alikua anakabiliwa mashtaka mawili ambayo ni  unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo, tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba 6, mwaka jana  katika eneo  la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam.

Mshitakiwa huyo pia anadaiwa kumwibia mali mlalamikaji zenye thamani   ya  kiasi cha shilingi 476,000.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni