Habari/News

Sababu za Sheikh Kishk kujiunga na mitandao ya Kijamii

Tarehe November 13, 2017

Sheikh Nurdeen Kishk Mkurugenzi wa Alhikma Foundation

[nafasi_ya_tangazo_la1

Mkurugenzi wa Al-hikma Foundation inayojishughulisha na masuala ya Elimu nchini Sheikh Nurdeen Kishk amesema kutokuwepo kwake kwenye mitando ya kijamii kumepelekea watu kumghasi wakitaka mahubiri yake na kazi zake ziweke kwenye mitandao ili iwafikie wanajamii wengi zaidi hasa vijana ambao wanatumia sana mitandao hiyo.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo Temeke Jijini Dar es Salaam Sheikh Kishk wakati akizindua KISHK ONLINE TV amekiri kwamba kutokana na kazi anayoifanya kuwa kubwa pamoja na Mahubiri anayo yatoa kwa jamii hana budi kujiunga na mitandao hiyo sasa huku akithibitisha kuwa na Online Tv.

“Tv hii haibagui na haiangalii waislamu na wasiokuwa waislamu kwani wanaonifatilia wako waislamu na wasiokuwa Waislamu”Amesema Sheik Kisk.

Amesema Tv hiyo itakuwa na Mihadhara mbalimbali, Hotuba za ijumaa, Usomaji wa Quran Tukufu pamoja na visa mbalimbali vitakavyo wajenga kiimani wale waliokata tamaa na kupoteza matumaini katika Imani.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni