Habari/News

Rushwa ya Soda yampandisha Kizimbani Mwenyekiti UVCCM

Tarehe December 11, 2017

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis akiwa Mahakamani leo mjini Dodoma.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis  amefikishwa Mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za Rushwa.

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amefikishwa leo Jumatatu Desemba 11,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa makosa mawili.

Kwa upande wake Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga alisema jana Jumapili Desemba 10,2017 kuwa Sadifa angefikishwa mahakamani leo akituhumiwa kuwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni