Habari/News

RC Kilimanjaro amng’oa kigogo ACT-Wazalendo

Tarehe June 11, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mghwira kikabidhiwa ilani ya CCM mbele ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mghwira kikabidhiwa ilani ya CCM mbele ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Act-Wazalendo Anna Mghwira kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya,  Bahati Longopa ametangaza kujiuzuluzu nafasi hiyo kwa kile alichodai kutoridhia uteuzi huo

Longopa amesema kuendelea kuwa kiongozi wa chama kutampa wakati mgumu kuhamasisha wanachama wapya katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Amesema kuwa kwa hiari yake ameacha nafasi hiyo ndani ya chama kutokana na kitendo cha viongozi wa juu wa Chama hicho kuingia ndani ya Serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya chama pinzani kwao na wao kama viongozi wa chini hawataweza kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na chama hicho.

Kuhusu kujiunga na chama  kingine cha siasa amesema kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo kwani ataendelea kukaa pembeni na kutojihususisha kwenye mambo ya siasa  huku akitafakari nini cha kufanya.

Naye Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Wilaya ya Mbeya, Ally Mbika amesema wamepata taarifa  za chini chini kuhusiana na kiongozi huyo, lakini kama chama bado hawajakabidhiwa barua yoyote kutoka kwa kada huyo kutamka kujiuzulu rasmi.

 Amesema  wanasubiri  kukabidhiwa  rasmi barua ili kuweza kulizungumzia kwa vyombo vya habari barua na  viongozi wa chama watapitia katiba yao na kupata mwongozo na kuangalia namna ya  kuziba nafasi hiyo mpaka Uchaguzi  Mkuu  wa  mwaka 2020.

Mbika amesema kuwa kujiengua kwa kada huyo ni pigo kwa chama kwani alikuwa ana mchango mkubwa wa ushawishi na kujenga umoja na mshikamano wa kweli wa ndani na nje ya mkoa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni