Habari/News

Ramaphosa anusa urais Afrika Kusini 2019

Tarehe December 19, 2017

Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini A-Kusini .

Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini A-Kusini  ambapo kwa sasa ameoneka kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Ramposa ambaye alikuwa makamu wa rais wa chama hicho aliweza kumshinda mpinzani wake Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura 2440 kwa 2161.

Cyril Ramposa alizaliwa tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio mwanasiasa tajiri zaidi Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni dola milioni 450.Tangu ujana wake Ramposa alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa shupavu na hiyo ndio ilimfanya kujiunga na uongozi wa chama cha wafanyakazi .

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni