Habari/News

Rais wa zamani Liberia ashinda tuzo ya Mo Ibrahim

Tarehe February 12, 2018

Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf .

Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika – ambayo hupewa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri.

Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.

Wakosoaji wake wamekuwa wakimkosoa kwa kuwa na upendeleo, kutokana na kuwachagua watoto wake katika nafasi za ngazi za juu na pia wanadai kuwa hakuchukua hatua za kutosha kupambana na rushwa.

Kamati ya utendaji ya Mo Ibrahimu imesema  kwamba inafahamu mapungufu yake, lakini imeamua kwamba anastahili kupata tuzo ya dola za kimarekani milioni 5.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni