Habari/News

Rais mpya Liberia aanza kwa Kumng’oa Waziri wa Sheria

Tarehe February 10, 2018

Rais mpya wa Liberia George Weah.

Rais mpya wa Liberia George Weah amemtimua kazi Waziri wa Sheria, Charles Gibson, kufuatia  malalamiko kuwa amepokonywa leseni ya uwakili baada ya kumtapeli mteja wake.

Inadaiwa kuwa  Kigogo huyo alipatikana na hatia hiyo na Mahakama ya Juu baada ya kumtapeli mteja wake Dola za Marekani elfu 25 na kuagizwa kuzirejesha

Rais Weah amemteua Musa Dean aliyekuwa Wakili katika Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi hiyo.

Rais Mwanasoka Bw Weah Liberia alichaguliwa kuwa Rais na kuchukua nafasi ya Bi. Ellen Johnson Sirleaf.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni