Habari/News

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi NBAA

Tarehe April 11, 2018

Rais John Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo tarehe 11 Aprili, 2018.

Prof. Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni