Habari/News

Rais Magufuli atangaza neema JWTZ, kumwaga ajira 3000

Tarehe September 23, 2017

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania.

Serikali inatarajia kutoa kibari kipya cha ajira kwa Wanajeshi 3000 wapya ili liweze kuwa na Askari wa kutosha kwa ajili ya ulinzi wa nchi na mipaka yake.

Hayo yamesemwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli  leo alipokuwa akihutubia umma mara baada ya kuwapa kamisheni maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

” Leo tumepata maofisa 422, unapokuwa na jeshi la maofisa lazima kuwepo na ‘junior officers’, huwezi ukawa na jeshi lote lina maofisa, kwa kutambua hili natangaza rasmi kwamba nitatoa nafasi 3,000 za kuajiri wanajeshi wapya, na hawa watakaoajiriwa muzingatie na wale ambao wamemaliza JKT, lengo ni kuhakikisha jeshi letu linakuwa na maaskari wa kutosha na la kisasa zaidi”, amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewataka Vigogo wa JWTZ kutowasahau vijana waliohitimu mafunzo ya JKT.

Rais Magufuli leo amevunja mwiko wa kufuatia kutoa kamisheni kwa Maafisa wa Jeshi 422 uwanja wa umma ambapo kamisheni hiyo imekua  ikitolewa katika chuo cha Monduli.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni