Habari/News

Rais Magufuli amteua Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu JWTZ

Tarehe February 14, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pamoja na uteuzi huo, Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;

Brig Jen. J.G. Kingu

Brig Jen. M.S. Busungu

Brig Jen. R.R. Mrangira

Brig Jen. B.K. Masanja

Brig Jen. G.T. Msongole

Brig Jen. A.F. Kapinga

Brig Jen. K.P. Njelekela

Brig Jen. A.S. Bahati

Brig Jen. M.E. Mkingule

Brig Jen. S.S. Makona

Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni