Habari/News

Rais Magufuli akerwa nchi kuwa kichaka cha fedha za kigeni

Tarehe December 13, 2017

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

(Weka Picha)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekerwa na kitendo cha kuingizwa fedha za kigeni kinyume cha sheria hapa nchini.

Akizungumza mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, Rais Magufuli amesema zaidi ya dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

“Ninapozungumza tu sasa hivi nimepata taarifa zaidi ya bilioni moja dola zimeshikwa Airport zilikuwa zinaingizwa Tanzania kwa sababu Tanzania kimeshaonekana ni kichaka cha fedha za kigeni” amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amezitaka Mahakama za Biashara kuharakisha kesi  za mikopo ili Benki ziendelee kutoa mikopo kwa watu wengine.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni