Habari/News

Rais Magufuli aizika rasmi hoja Mbunge wa CCM

Tarehe January 14, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amefunga rasmi mjadala kuhusu hoja  iliyoibuliwa na Mbunge wa Kondoa Juma Nkamia aliyetaka kupeleka muswada Bungeni  akitaka muda rais kukaa madarakani uongezwe.

Rais Magufuli amefunga mjadala huo  jana wakati alipokutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  IKulu, ndg. Humphrey Polepole na kumtuma awajulishe watanzania na wana CCM kwamba wapuuze mijadala hiyo kwani jambo hilo halijawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Ikulu, Rais Magufuli amemuagiza Polepole kuwajulisha watanzania na wana CCM kuwa wasikubali kuyumbishwa au kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2017.

Kufuatia Rais Magufuli  kuweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kutoka miaka 5-7 na pia hafurahishwi na mijadala hiyo ni wazi sasa hoja ya Mbunge Nkamia haina mashiko na sasa watanzania  hawana budi kuacha kushabikia mjadala huo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni