Habari/News

Rais Kenyatta naye kukimbilia mahakamani kama Odinga

Tarehe October 13, 2017

Uhuru Kenyatta.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa anakusudia kukata rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu ya kumjumuisha Dkt. Ekuro Aukot katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa marudio baada ya ule wa awali kufutiliwa mbali.

Kupitia kwa Mwanasheria wake Tom Macharia, Rais Kenyatta aliiambia Mahakama kuwa anakusudia kwenda kwenye Mahakama ya Rufaa Jumatatu ijayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya maombi katika hukumu ya Mahakama Kuu kumruhusu Dkt. Aukot kugombea Urais kutangazwa na Justice John Mativo.

Jumatano, Justice Mativo alisema kuwa Dkt. Aukot lazima ajumuishwe kwenye uchaguzi wa marudio ambao umepangwa kufanyika October 26, 2017.

Mahakama ilikwenda mbali zaidi kuieleza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kurekebisha katika maandalizi yao na kumjumuisha Dkt. Aukot kama mgombea.

Kufuatia uamuzi huo Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya, IEBC ilisema kuwa sasa itajumuisha wagombea wa Urais wote walioshiriki katika kinyang’anyiro cha mwanzo na kwamba kama kuna ambaye atataka kujitoa atawasilisha barua na fomu maalum katika tume hiyo kuthibitisha kujitoa.

Tayari mgombea wa Urais kupitia NASA, Raila Odinga ametangaza kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutofanyiwa marekebesho kwa baadhi ya mambo ikiwemo tume hiyo ambayo iliharibu uchaguzi wa awali.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni