Habari/News

Rais Duterte atishia kuwaua Mameya nchini mwake

Tarehe January 11, 2017

c14p_uywiaew3sh

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amewaonya Mameya mafisadi nchini humo kuchagua kujiuzulu au  kufa kama watakuwa katika orodha ya washukiwa wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Duterte, 71, ameyasema hayo mbele ya Mameya zaidi ya 200 waliochaguliwa pale walipokuwa wakila kiapo akiwaambia ni afadhali wakajiuzulu na kujisafisha au atahakikisha anawaua.

“Nitawaita mameya wote na kuwafungia ndani ya chumba na itakuwa ni sisi peke yetu. Nitawaambia angalieni orodha hiyo nene niliyowapa kama kuna jina lako, na kama kuna jina lako basi utakuwa na tatizo kubwa kwasababu nitakuua,” amesema Duterte.

Rais huyo amewahi kukaririwa akisema kuwa Mameya nchini humo wanahisiwa kutumia madaraka yao kuhakikisha maafisa wa polisi hawaingilii mienendo yao ya biashara ya madawa katika miji mikubwa na itaa nchini humo.

Mara kadha ametahadharisha kuwaua watu wote wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni