Habari/News

Polisi yamuachia kwa dhamana ‘Bilionea Dkt. Louis’, asisitiza msimamo wake

Tarehe November 14, 2017

Dkt. Luis Shika.

Mtu aliyejipatia umaarufu ndani ya siku chache zilizopita baada ya kuvuuga mnada wa nyumba za Mfanyabiashara, Said Lugumi, Dkt. Louis Shika ameachiwa na polisi baada ya kujidhamini mwenyewe baada ya kukaa rumande kwa siku kadhaa.

Dkt. Shika ambaye anasadikika kuwa na matatizo ya akili alipanda daladala mara baada ya kuachiwa na polisi na kwenda nyumbani kwake huku akisisitiza  kuwa bado mpango na dhamira yake ya kununua nyumba hizo ipo palepale kwani Kampuni yake ina uhitaji mkubwa wa nyumba hizo.

Amesema anasubiri fedha zake ziweze kuingizwa katika akaunti yake na kulipa asilmia 25 inayotakiwa kama masharti ya mnada na kuitaka Kampuni ya Yono na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuita waandishi wa habari ili waone atakavyolipa na kuutangazia umma.

Hatahivyo mnada huo ambao ulivurugwa na Dkt. Louis baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 ya nyumba tatu za Lugumi baada ya kuwa mshindi unatarajiwa kufanyika tena siku nyingine kama itakavyopangwa na Yono Auction Mart.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni