Habari/News

Polisi waibua sababu Diwani wa Chadema kuawa kwa Mapanga

Tarehe February 24, 2018

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema kuwa mauaji ya Diwani wa Kata ya Nawala tarafa ya Ifakara wilayani Kilombero, Godfrey Joackim (CHADEMA) ni kutokana na kulipa kisasi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi, Urich Matei amesema kuwa kiongozi huyo kuna wakati aliwahi kuwaambia wanakijiji kuwa mtu ambaye alikuwa anafahamika kwa jina la Kenani Haule ndiye alikuwa anawasaliti hivyo baada ya muda mtu huyo aliuliwa kwa kupingwa mapanga.

Watu wa  Nawawala walikuwa na ugomvi kati ya wanakijiji na bodi ya sukari akiwa diwani wa eneo lile alisimamia wananchi wale kudai lile shamba, kuna kesi ambayo ipo mahakamani mpaka sasa inaendelea lakini aliwaambia mtu mmoja anaitwa Kenani Haule ndiye tatizo, kwa hiyo diwani Godfrey Joackim aliwaambia tu kuwa huyo Haule ndiye anawasaliti.” amesema Matei

“ Hivyo aliwaambia hata kama Kenani akifariki basi wao watakuwa na uwezo wa kupata shamba na kweli muda mfupi Kenani Haule aliuawa kwa kukatwa katwa mapanga tukio ambalo lilitokea kama lilivyotokea kwake, kimsingi kabisa tunaamini Godfrey Joackim atakuwa ameuawa kwa ajili ya kisasi baada ya kifo cha Kenani Haule” ameongeza Matei

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni