Habari/News

Polisi wabaini ‘siri’ ya Mnunuzi Nyumba za Lugumi

Tarehe November 10, 2017

Dkt. Luis Shika.

Mnunuzi wa nyumba za lugumi zilizopigwa mnada jijini Dar es salaam jana Dk. Louis Shika  imebainika kuwa alitumwa na Lugumi mwenyewe ili kukwamisha nyumba zake zisiuzwe.

Hayo yamebainishwa na Jeshi la Polisi jijini Dares salaam ambapo Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linahisi kuwa alitumwa na Lugumi kutokana na mazingira ya tukio husika.

Amesema Dk. Louis ambaye alifunga mnada wa nyumba hizo kwa kuahidi kulipia shilingi milioni 900, alishindwa hata kutoa robo ya kiasi hicho kwa mujibu wa masharti ya mnada hali iliyopelekea kufikishwa katika kituo cha polisi.

“Ingawa sina facts (vielelezo) kuthibitisha hilo, lakini alichokuwa anafanya kinatufanya tuamini hivyo. Kwasababu alikuwa anapandisha bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” aliongeza.

Inadaiwa kuwa muonekano wa Dkt Shila pia ulikuwa unatia shaka na kwamba Jeshi hilo linaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi.

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kupitia Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) jana ilitangaza  kuuza nyumba mbili mali ya Lugumi kwa gharama ya Tsh 1.9 bilioni.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni