Habari/News

Polepole awataka waliokosa mikopo elimu ya juu wamtafute

Tarehe January 5, 2017

Humphrey PolePole

Humphrey PolePole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humprey Polepole amewatangazia neema wanafunzi wa elimu ya juu waliokosa mikopo, akiwataka wamtafute ili awaoneshe cha kufanya

Akizungumza kuhusiana na tatizo la mikopo elimu ya juu katika kituo kimoja cha luninga nchini, Polepole amedai kuwa Serikali imekwishatoa maelekezo kwamba haiwezi kumkopesha kila mtu na kwamba inatoa mikopo kwa vigezo vilivyowekwa.

Kuhusu watu wasioweza kujigharamia elimu hiyo na wamekosa mikopo, amewashauri kuahirisha masomo yao, ili wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata pesa na ndani ya mwaka mmoja ana uhakika watakuwa wamepata pesa zinazohitajika na kuendelea na masomo yao.

Polepole ametaja baadhi ya shughuli ambazo angewashauri wazifanye kuwa ni pamoja na kilimo huku akitolea mfano baadhi ya watu aliowashauri wajiingize kwenye kilimo cha matikiti na wakaufanyia kazi ushauri huo, ambapo baada ya muda wameona matunda yake.

“Waliokosa mikopo vyuo vikuu wanitafute, nitawaonesha cha kufanya, na wawe tayari kuahirisha masomo mwaka mmoja,” amesema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni