Habari/News

Polepole atoa sababu kukwama mchakato wa Katiba Mpya

Tarehe October 12, 2017

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema mchakato wa Katiba Mpya ulikwama kwa sababu hakukuwa na uelewa wa pamoja nini wananchi wanataka jambo ambalo tayari limeshaeleweka ndani ya chama hicho.

Polepole amenukuliwa akisema hayo leo katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini na kusisitiza kuwa yeye ni muumini wa maoni ya wananchi kwenye mchakato wa Katiba Mpya.

Amesema wakati ya mchakato wa Katiba Mpya alikuwa miongoni mwa wajumbe waliokusanya maoni ya wananchi hivyo ataendelea kuunga mkono maoni yao.

“Nilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima ya Tanzania na ninajua nini Watanzania wanasema kwa hiyo, mimi ni muumini wa maoni ya wananchi,” amesema.

Amesema mchakato huo ulikwama kwa sababu hakukuwepo na uelewa wa nini Watanzania wanataka.

Hata hivyo amedai kuwa mabadiliko makubwa yanayofanywa ndani ya chama hicho yanaakisi kushughulikia kero za wananchi.

“Siasa safi ni kushughulika na kero za wananchi wetu, chama kimejitathmini na kujisahihisha kwa sababu tumepata ushahidi kwamba kuna mahali tulikosea kwa hiyo, tunao utaratibu wa kujikosoa,” amesema.

Polepole amesema uongozi wa  Rais, Dkt. John Pombe Magufuli umejikita zaidi katika kushughulikia kero za wananchi kwa kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uadilifu huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni