Habari/News

Pole Pole afichua siri Mkutano wa Dharura Chadema

Tarehe December 7, 2017

Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.

Wakati chama cha Chadema waki itisha mkutano wa dharula wenye ajenda mbalimbali ikiwemo kujadili uchaguzi wa majimbo wa marudio na kata ifikapo januari 13,2018,Katibu Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amefichua siri ya mkutano huo.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Polepole amesema CHADEMA wamefanya kikao cha dharura  kususia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata unaotarajiwa kufanyika Januari 13 mwakani.

Ameongeza kuwa  ukweli ni kwamba Chadema  wamefulia baada ya kutumia vibaya hela ya mfuko wa chama chao.

Amesema  CHADEMA  wanatumia mgongo wa kuminywa kwa Demokrasia nchini kususia uchaguzi huo kitua ambacho sio sawa.

“Watani wanakutana leo, ajenda ni kutoshiriki uchaguzi unaokuja wa marudio kwa kisingizio cha demokrasia lakini ukweli ni matumizi mabaya ya fedha yamefuja mfuko wa chama. Tafuteni visingizio vingine lakini sio demokrasia. Watu wamechoka siasa za matukio. Kikao chema!” Ameandika polepole katika ukurasa wake wa Twitter.

Chama cha Chadema kilitangaza kususia uchaguzi wa marudio katika baadhi ya kata kwenye uchaguzi wa madiwani  jimbo la Arumeru kwa madai ya kuwepo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikwemo Mawakala kukamatwa na Jeshi la Polisi na  kuibuka vurugu wakati wa kuhesabu kura.

Katika  uchaguzi  huo CCM  ilishinda kwa kishindo ambapo katika jimbo la Arumeru Mashariki ilipata kata nne.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni