Habari/News

Picha:Rais Magufuli alivyoshiriki Misa ya Jumatano ya Majivu

Tarehe February 14, 2018

Rais John Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14.

Dar es salaam,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  leo ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu.

Ibada ya misa ya Jumatano ya Majivu inaashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.

Ibada hiyo imeongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph.

Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu wakati wa ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni