Habari/News

Obama atoa hotuba ya mwisho akiwahimiza wamarekani kutetea demokrasia

Tarehe January 11, 2017

 

_93352594_bac2fe63-877b-49be-8b2a-da108a246cfd

Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, katika hotuba yake ya mwisho kama Rais wa Marekani aliyoitoa Mjini Chicago.

Amewaomba Wamarekani wa kila asili kupambanua mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba “lazima tuwategee sikio wengine na kusikia”.

Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.

Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55 na ataapishwa tarehe 20 Januari.

“Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka,” amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika Mjini humo.

Hata hivyo ameongeza kuwa, “demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani”.

Umati wa watu ulisema kwa sauti “miaka minne zaidi” lakini kiongozi huyo alipuuzia mbali na kusema “Siwezi kufanya hivyo.”

Marais wa Marekani wanaruhusiwa kuongoza kwa mihula miwili pekee katika katiba.

Ameishukuru familia yake kwa kujinyima mambo mengi kutokana na nafasi waliyonayo.

Ameishukuru familia yake kwa kujinyima mambo mengi kutokana na nafasi waliyonayo.

Bw Obama, aliyeonekana mchangamfu, alisema utamaduni wa kukabidhi madaraka kwa warithi kwa njia ya amani ni moja ya mambo makuu yanayotambuliwa katika demokrasia Marekani.

Lakini amesema kuna mambo matatu yanayotishia demokrasia Marekani – ukosefu wa usawa kiuchumi, mgawanyiko kwa misingi ya rangi na hatua ya baadhi ya makundi kwenye jamii kujitenga na kuwa na misimamo ambayo haiongozwi na ukweli.

Akikamilisha hotuba yake, amesema ombi lake moja la mwisho kabisa kwa Wamarekani akiwa kama rais ni: “Nawaomba muwe na imani. Si katika uwezo wangu wa kuleta mabadiliko – bali katika uwezo wenu.”

Obama alikuwa amerejea Chicago, mahali ambapo alitangaza ushindi mwaka 2008 na kutoa hotuba iliyokuwa na ujumbe mkubwa wa matumaini baada ya kipindi cha kampeni za mgawanyiko kati ya Bw Trump na Bi Hillary Clinton.

Bw Obama amesema Wamarekani wengi wa umri mdogo, wakiwemo wale walioshiriki kampeni zake na wanaoamini katika “Marekani ya usawa, haki na inayojumuisha watu wote” wanampa matumaini zaidi sasa kuliko wakati alipoanza.

Rais Obama amesema Makamu wa Rais Joe Biden amekuwa kama ndugu kwake

Rais Obama amesema Makamu wa Rais Joe Biden amekuwa kama ndugu kwake

Kwa kuchagua Chicago, Bw Obama amesema awali kwamba alitaka kurejea mahala ambapo “mambo yote yalianzia” kwake na Mkewe Michelle Obama, badala ya kutoa hotuba yake hiyo kutoka Ikulu ya White House.

“Hotuba hiyo iliandikwa kwa wazo la kuwazungumzia Wamarekani wote, wakiwemo wafuasi wa Trump,” maafisa wake wamesema.

Ziara hiyo ya Bw Obama Mjini Chicago ndiyo yake ya mwisho kama Rais, na safari yake ya 445 akiwa amesafiri ndege ya Rais ya Air Force One.

Watu zaidi ya 20,000 walitarajiwa kuhudhuria hotuba hiyo katika ukumbi wa mikutano wa McCormick Place, ambao ndio mkubwa zaidi Amerika Kaskazini na ukumbi ambao Bw Obama alitoa hotuba mwaka 2012 baada ya kumshinda Mitt Romney uchaguzi wa 2012.

_93352481_352dd32a-9c8f-4046-b640-f807a60d366f

Tiketi zilitolewa bila malipo lakini kuna watu walikuwa wanaziuza $1,000 (£820) mtandaoni saa chache kabla ya hotuba yake kuanza.

Umekuwa ni utamaduni kwa rais kutoa hotuba ya mwisho Marekani kwa muda mrefu.

Marais wa zamani George W Bush na Bill Clinton walitoa hotuba zao kutoka White House, lakini George Bush Snr alitoa hotuba yake kutoka chuo cha jeshi cha West Point.

Anapoondoka madarakani, Rais Obama anaungwa mkono na 57% ya Wamarekani, kwa mujibu wa kura ya maoni ya Associated Press-NORC Center for Public Affairs Research poll, kiwango sawa na cha Bill Clinton alipokuwa anaachia madaraka.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni