Habari/News

NEMC watangaza Bomoa Bomoa nchi nzima

Tarehe August 28, 2017

Bomoa  Bomoa ilivyotikisa bonde la Mto Msimbazi.

Bomoa Bomoa ilivyotikisa bonde la Mto Msimbazi.

Baada ya Bomoa Bomoa kubwa kutikisa  Barabara ya Morogoro eneo la Kimara na  kuwaacha baadhi ya watu bila makazi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetangaza Bomoa Bomoa nyingine  nchi nzima kwa wananchi waliovamia na kujenga kando ya Mito na Bahari.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini hapa,Mwanasheria  wa NEMC Manchare Heche amesema  wananchi waliofanya makazi katika maeneo hayo wanapaswa kuondoka kabla ya kuvunjiwa kwa nguvu.

Licha ya kutotaja siku ya kuanza bomoa bomoa hiyo Manchare alisema wananchi waliojenga katika maeneo hayo hatarishi wanapaswa kuondoka kabla ya kuchukuliwa hatua  na serikali.

Hadi sasa mamia ya Wananchi wamekosa makazi maeneo ya Kimara hadi mbezi kufuatia Wakala wa Barabara kuwataka wananchi hao kubomoa nyumba zao kwa kuwa wamejenga ndani ya hifadhi ya Barabara.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni