Habari/News

NEC:’Chadema wakijitoa,CCM itapita bila kupingwa’

Tarehe December 12, 2017

Wakati uchaguzi mdogo ukipangwa kufanyika januari 13,2018 katika majimbo matatu na kata sita,Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema endapo chama cha siasa kimoja kitagoma kufanya uchaguzi,chama kingine kitapita bila kupingwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.Kailima Ramadhan amesema Tume ya uchaguzi  nchini haiko kwa ajili ya kumshawishi mtu au chama  kushiriki kwenye uchaguzi huo.

“Iwapo kuna chama kitaamua kutoshiriki uchaguzi,kitakachoshiriki hata kama ni kimoja mgombe wake atapita bila kupingwa”Imesema taarifa ya Kailima.

Kauli ya Kailima inafuatia chama cha Chadema kutangaza kususia uchaguzi wa marudio kwa madai kwamba kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi katika uchaguzi wa marudio wa madiwani.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema Ukawa itajitoa katika uchaguzi huo endapo  Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitazifanyia kazi changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita.

Katika uchaguzi huo vyama vya Chadema na CCM vitachuana vikali,ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu CCM ishinde kwa kishindo kwenye uchaguzi wa marudio.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni