Habari/News

Ndege ya Kijeshi Algeria yaanguka na kuua watu 257

Tarehe April 12, 2018

Ndege iliyopata ajali.

Takriban watu 257 wamefariki baada ya ndege ya kijeshi kuanguka kaskazini mwa Algeria , kulingana na wizara ya ulinzi.

Ajali hiyo imetokea muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufariki karibu na mji mkuu wa Algiers asubuhi.

Wengi wa waliouawa ni wanajeshi na familia zao kulingana na wizara ya ulinzi huku wafanyikazi 10 wa ndege hiyo pia wakifariki.

Haijulikani ni nini haswa chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo. Afisa mkuu wa jeshi ameagiza uchunguzi wa ndege hiyo na atatembelea eneo la mkasa.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni