Habari/News

NBS yafunguka hali ya mfumuko wa bei

Tarehe May 8, 2018

Mfumuko wa Taifa wa bei kwa mwezi april 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.8 ikilinganishwa  na asilimia 3.9 ilivyokuwa  mwezi machi 2018.

Hayo  yamesema  na  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na  Waandishi wa Habari jijini hapa na kubainisha kuwa  kasi ya Mabadiliko ya bei za Bidhaa na huduma kwa mwaka ulioshia mwezi April 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulio ishia mwezi machi 2018.

Amesema kupungua kwa kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioshia mwezi April 2018 kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bidhaa za Vyakula.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya April 2017 na April 2018 ni pamoja na Mahindi kwa asilimia 5.2,unga wa Mahindi kwa asilimia 5.6,Mtama kwa asilimia 5.6,mtama asilimia 7.3,unga wa Mihogo kwa asilimia 9.3. Maharage kwa asilimia 9.2 na mihogo mibichi kwa asilimia 13.2.

Kwa upande wa Afrika Mashariki Kwesigabo amesema,Nchini Uganda  mfumuko wa bei ulioshia mwezi April 2018 umepungua hadi asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.0 kwa mwaka ulioshia mwezi machi 2018,na Nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi April 2018 umepungua hadi asilimia 3.73 kutoka asilimia 4.18 kwa mwaka ulioshia mwezi machi 2018.

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni