Habari/News

Nassari: Mtuhumiwa sakata la madiwani atumia ‘sangoma’ kujizatiti

Tarehe October 12, 2017

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Wakati sakata la kununuliwa kwa madiwani wa Chadema Mkoani Arusha na kuhamia CCM likiwa limeshatua mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Mhe. Joshua Nassari ameibuka tena na kudai mtuhumiwa mmojawapo wa sakata hilo ameanza ‘kujizatiti’ kwa kushirikisha nguvu za giza.

Nassari ametumia mitandao ya kijamii kuandika yafuatayo;

“Mmoja wa watuhumiwa wa rushwa ya ununuzi wa Madiwani wa Arumeru aishie maeneo ya Mukidoma Usa-River ameleta mganga toka kanda ya ziwa, na yupo nyumbani kwake. Lengo ni kumsaidia mtuhumiwa huyu asipoteze ajira yake. Mganga huyu ameletwa na mama wa mtuhumiwa. Tutaanika hadharani acha tuone tofauti ya Mungu na miungu.”

Hivi karibuni Mhe. Nassari akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Mhe. Godbless Lema waliibuka na kudai kuwa wana ushahidi wa madiwani hao kununuliwa, ambao walionesha sehemu ya ushahidi huo kwa waandishi wa habari, na siku iliyofuatia waliwasilisha ushahidi huo ulio katika ‘flash’ katika taasisi husika ya Takukuru.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni