Habari/News

Nassari adaiwa kumshambulia Mtendaji,afikishwa Mahakamani

Tarehe February 6, 2018

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema).

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

Mbunge huyo  amefika Mahakamani  hapo   akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.

Akizungumzia tukio hilo  Nassari amesema jana alikwenda Kituo cha Polisi Usa River kufuatilia silaha yake iliyochukuliwa na askari wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014.

Amesema alipofika polisi alielezwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtendaji kosa analodaiwa kutenda mwaka 2014 .

Naye  wakili wa Nassari Sheki Mfinanga amesema hajui mteja wake anakabiliwa na shtaka gani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni