Habari/News

Nape:’Upinzani wasahau kuiangusha CCM’

Tarehe January 13, 2018

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye.

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye amesema  wapinzani nchini wasahu kuiangusha CCM katika chaguzi mbalimbali nchini.

Akizungumza alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombe ubunge wa jimbo la Longido kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambao unatarajiwa kufanyika leo Januari 13, 2018 Nape amesema CCM inapofika wakati wa kutafuta dola hawana urafiki na mtu.

“Ikifika wakati wa kutafuta dola CCM inakuwa kitu kingine kabisa, unaweza kuichezea wakati wa kawaida na tunaweza kupiga stori ila ikifika kwenye kutafuta dola hapo ni mambo mengine kabisa. Ndiyo maana nasema wenzetu watasubiri sana kwani haiwezekani kuiangusha CCM madarakani alisisitiza Nape Nnauye

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni