Habari/News

Nape afunguka Sugu kutoka Gerezani

Tarehe May 10, 2018

Nape Nnauye mbunge wa Mtama.

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kumkaribisha uraiani Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliyeachiwa baada ya kumaliza kifungo gerezani.

Kupitia ukurasa wa Twita Nape amesema

“Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter.

Sugu pamoja na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walifungwa baada kudaiwa utoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli.

Inadaiwa kuwa Vigogo hao wa Chadema walitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni