Habari/News

Mwigulu aonya watakaochangisha fedha uandikishaji Vitambulisho

Tarehe February 3, 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba amewataka watanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambuliwa.

Waziri Mwigulu amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania .

“Zoezi hili ni bure kujiandikisha na kupata kitambulisho pasitokee kiongozi yeyote wa wilaya na vijiji kuchangisha fedha wananchi ili wapate fomuza kujiandikisha na wala zoezi hili lisiunganishwe na siasa.”alisema Dr.Mwigulu

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni