Habari/News

Mwenyekiti wa zamani CCM Dar,wenzake 5 wapata dhamana

Tarehe December 15, 2017

Mwenyekiti wa CCM Ramadhani Madabida.

Mwenyekiti wa CCM  wa zamani  Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida  na wenzake watano leo wamepata dhamana na kuachiwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hatua hiyo inafuatia  Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa ambapo wanakabiliwa mashtaka  mawili ni ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaominika, kila mdhamini akisaini bondi ya Sh 12 milioni,wametakiwa watoe fedha taslimu Sh 12 milioni ama mali isiyo hamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni