Habari/News

Mwanamke aliyetelekezwa na Mchina azua mapya

Tarehe April 11, 2018

Mwanamke aliyetelekezwa na Mchina Bi Safina Mohamed amezua mapya baada ya kuvishushia lawama vyombo vya habari kwa kusambaza picha ya mtoto wake.

Safina amesema kitendo cha kusambazwa picha ya mtoto wake ni kinyume na maadili kwa kuwa yeye dhamira yake ni kutafuta haki ya mtoto wake.

Nia na malengo na madhumuni ya kunileta hapa ni kutafuta haki ya mtoto wangu, kama watoto wengine ambao wakiafrika waliotelekezwa kwa maana hiyo nasikitika sana kwa mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa ambazo ni tofauti na zile zilizonileta hapa, na nasikitika kwa nini picha za mtoto wangu zinasambazwa? kwa hiyo naomba jamii isinichukulie mimi vibaya mimi nataka haki ya mtoto wangu,“amesema Bi. Safina

Akizungumzia kuhusu kuetelekezwa Safina amesema na mumewe aliyemtaja kwa jina la Zhou Quin aliyeondoka nchini baada ya kibali chake cha kufanya kazi nchini kuisha mwaka 2016, na mpaka sasa hana mawasiliano naye.

Wanawake wengi wame endelea kumiminika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni