Habari/News

Mwalimu aumizwa kuibuka hoja ya Uzanzibar

Tarehe February 11, 2018

Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu.

Hoja ya Uzanzibar ime endelea kumtafuna  Mgombea wa Ubunge wa  jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu kufuatia  kutajwa kwenye kampeni za uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hoja hiyo Mwalimu amesema baadhi ya watu kuibua hoja ya uzanzibar kwa sasa kunaweza  kulipasua Taifa.

Amesema wakati wa vita zinatumika silaha mbalimbali lakini ni vema kwenye hili la la kuleta Utanganyika na U-zanzibar likatumiwa kwa tahadhari ili lisije kuleta madhara.

Mwalimu amesisitiza kuwa hajawahi kuuficha utambulisho wake na kwamba yeye ni ni mzaliwa wa Zanzibar na wala haoni kama ni jambo la ajabu.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni