Habari/News

Mwalimu anaswa ‘guest’ akifanya Mapenzi na Mtoto wa Shule

Tarehe August 7, 2017

miaka 30

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35) amepandishwa kizimbani katika  Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato cha nne, Kata ya Mwisi.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya mapenzi na mwanafunzi wa mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa).

Hata hivyo  Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni