Habari/News

Mvua ya mfululizo yatikisa Dar,watu 7 wafariki dunia

Tarehe April 16, 2018

Mvua za mfululizo zinazoendelea kunyesha jijini Dares salaam zimepelekea watu saba kufariki dunia.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa na kubainisha kuwa mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.

Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.

“Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo”Amesema Mambosasa

Amesema Jeshi la Polisi  litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali kuhusu hali ya mvua, ambayo inaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.

“Kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, ameongeza Kamanda Mambosasa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni