Habari/News

Mvua kubwa yatabiriwa kutikisa Dar na Pwani

Tarehe May 9, 2018

Hatimaye baada ya mvua kutikisa katika maeneo ya Dar es salaam na kusababisha mafuriko, Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini (TMA)imetoa utabiri mwingine.

Kwa mujibu wa utabiri huo umeeleza kuwa kiwango hicho cha mvua kilitarajiwa kuanza jana usiku. Mvua hiyo  inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Kiwango cha mvua hiyo kitaendelea kwa siku tano na wanaoishi mabondeni, wametakiwa kuchukua tahadhari.

TMA imeeleza kwamba athari zinazoweza kutokea ni mafuriko ambayo yatasababisha msongamano wa magari na watu hali itakayochelewesha usafiri na usafishwaji maeneno ya mjini.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni