Habari/News

Muhongo asikitishwa na kusuasua ujenzi bomba la mafuta Tanzania-Uganda

Tarehe January 10, 2017

ugandapick

Serikali ya Tanzania imeelezea kutoridhishwa kwake na kusuasua kwa mipango ya kujenga bomba la mafuta likiunganisha nchi ya Tanzania na Uganda.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa uzinduzi wa tafiti ya Front-End Engineering Design (FEED) kwa ajili ya mradi huo.

“Hadi sasa tumepiga hatua chache sana kuelekea ukamilishwaji wa mradi huo na sina raha kuhusiana na mwendo wa mradi huu,” amesema Muhongo.

FEED inajielekeza katika mahitaji ya kiufundi ili kutoa picha halisi ya mradi huo na kuhakikisha kuwa maamuzi ya mwisho ya uwekezaji huo ‘Final Investment Decision’ yanafikiwa mwishoni mwa mwaka 2017 ili kutoa njia ya kuanza ujenzi mapema mwaka 2018.

Mradi huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 3.55 (sawa na shilingi trilioni 12).

Naye Waziri wa Madini wa Uganda, Irene Muloni amesema kuwa tafiti za FEED zitakwenda sambamba na tafiti zingine kama Ressetlement Action Plan (RAP) na Environmental and Social Impact Assessments (ESIAs) huku kukiwa na mtazamo wa kuharakisha mradi huo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni