Afya

Muhimbili yaweka Historia kwa upandikizaji wa figo

Tarehe November 25, 2017

Muhimbili yaweka Historia kwa upandikizaji wa figo

 

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na hospitali ya BLK ya New Delhi, India kwa mara ya kwanza  imefanikiwa  kufanya upasuaji wa kihistoria wa upandikizaji wa figo (Rnal Transplant ).

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Dkt, Ummy Mwalimu  amesema kwamba upasuaji huo ni juhudi za serikali kuokoa fedha ambazo zingelipwa nje ya nchi kugharamia matibabu hayo na badala yake fedha hizo zitumike kuleta maendeleo kwenye maeneo mengine yenye uhitaji nchini.

Ameongeza kwamba zaidi ya mwaka Hospitali ya Taifa ilijikita kuwekeza kwenye kuongeza ujuzi wa wataalamu wa aina mbalimbali  wakiwemo wa upasuaji wa kupandikiza figo  na kwamba wataalamu 19 walipelekwa nchini India, na Norway kwa ajili ya utaalam, wa mafunzo hayo.

Upandikizaji figo ikiwemo vipimo mbalimbali vinavyohitajika kwa mpokeaji figo na mtoaji unagharimu takribani milioni 21.

Hapo awali  serikali ilikuwa ikigharamia milion 80-100 kwa mgonjwa mmoja huku ikidaiwa kwa mwaka walikuwa wanasafirishwa wagonjwa hadi 35 kwenda nje ya nchi kupata matibabu hayo.

Takribani wagonjwa 400 wanakadiriwa kuwa katika huduma hii katika vituo mbalimbali hapa nchini ambapo kwa hospitali ya Muhimbili wanaopata huduma kwa sasa wapo 200 na waliobakia ni wapo katika vituo mbalimbali vya Serikali na Binafsi

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni