Tarehe June 19, 2017
Shirika moja la ndege la binafsi nchini India limemtunuku safari za bure mtoto aliyezaliwa ndani ya moja ya ndege zake, iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea nchini India.
Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama mmoja kujifungua mtoto umbali wa futi 35,000 angani.
Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya ndege ya Boeng 737 kutua katika Mji wa Magharibi wa Mumbai.
Shirika hilo liliiambia BBC kuwa mama na mtoto wake walikuwa katika afya nzuri.
Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama kujifungua salama.
Shirika hilo lililisema kuwa hiyo ndiyo mara ya kwanza mtoto kuzaliwa kwenye ndege yake.
Lakini mashirika kadhaa yamekumbana na hali kama hiyo. Wahudumu wa Shirika la Ndege la Uturuki walisherehekea kuzaliwa kwa mtoto msichana ndani ya ndege mwezi Aprili mwaka huu.
Maoni