Habari/News

Msigwa amvaa Kigwangalla kuitaka Takukuru imchunguze Nyalandu

Tarehe November 14, 2017

Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa.

Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kuifahamu wizara anayoifanyia kazi na siyo kutafuta kujulikana kitu ambacho hakiwezi kudumu.

“Kigwangalla anatafuta kick ambazo haziwezi ku- last ! Brother take time to know the Ministry! Be humble and show your talents! You will be respected!” Msigwa

Msigwa amesema hayo Kupitia mtandao wake wa  Twita na kumsisitiza kuwa Waziri Kigwangalla  aonyeshe uwezo wake na kuwa mpole ili aje kuheshimika.

Kauli ya Msigwa inafuatia Waziri wa Kigwangalla kulitaka jeshi la Polisi na TAKUKURU kumchunguza aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Lazaro Nyalandu, kwa kutumia madaraka yake vibaya wakati wa uongozi wake.

Waziri Kingwangalla amedai kuwa katika uongozi wake Nyalandu ali ishi kama Malaika ambapo ali isababishia hasara Serikali kwa kiasi cha bilioni 32.

Inadaiwa kuwa Nyalandu ana andamwa kufuatia uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi ya Ubunge na kujivua uanchama CCM na kuhamia chama cha Chadema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni