Habari/News

Msemaji Serikali: Rais Magufuli hajakataa ongezeko la mishahara watumishi wa umma

Tarehe October 13, 2017

Dkt. Hassan Abbas.

Serikali imesema kuwa hakuna mahali Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipokataa kutekeleza ahadi ya ongezeko la mwaka la mishahara ya watumishi wa umma.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Dkt. Hassan Abbas alipokutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yahusuyo utumishi wa umma ambayo yamejitokeza hivi karibuni.

Amesema kuwa Rais alichokataa ni kuongeza Posho za Madiwani kutoka 350,000 hadi 800,000/= ambayo ni sawa na ongezeko la 150%.

Aidha, amedai kuwa tangu Julai 2017 mpaka sasa, Serikali imelipa Madeni ya Watumishi wa Umma ya Shilingi Bilioni 37.4 na itaendelea kulipa.

Hivi karibuni akiwa anahutubia Mkutano wa ALAT, Rais Magufuli alikaririwa akisema kuwa hakuna nyongeza ya mshahara kwakuwa Watanzania wengi bado wanahitaji huduma muhimu za maendeleo baada ya madiwani kutoa ombi hilo la kuongezewa mishahara.

Kauli hiyo ilizua mijadala mingi katika maeneo tofauti tofauti, hasa katika mitandao ya kijamii, huku Serikali ikishutumiwa kwa kukataa kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma iliyo katika sheria ‘Annual Increment’.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni