Habari/News

Mrema kula sahani moja na aliyemzushia ‘kifo’

Tarehe January 12, 2018

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Mrema alipowasili kuripori kuhusu kuzushiwa kifo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Mrema  amefika kituo cha Polisi jijini Dar es salaam  na kuripoti kuhusu mtu aliyemzushia kifo  Januari 9 mwaka huu kupitia mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  leo Mrema  amesema aliyezusha taarifa hiyo alifahamu kwamba Lowassa amekwenda Ikulu kuonana na Rais Dkt Magufuli, hivyo akazusha uongo ili watu wasiwe makini kuhusu kilichojadiliwa Ikulu.

Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kumchukulia hatua aliyezusha taarifa za kifo chake ili iwe fundisho kwa wengine.

Amesema wapinzani wa Rais ndio walizusha taarifa hizo za uongo na kuzua taharuki kwa sababu yeye ni mtu maarufu na wanajua kwamba kwa kufanya hivyo wangesababisha watu kutofautilia kilichozungumzwa Ikulu.

Kuhusu fidia Mrema amesema anataka kulipwa fidia ya shilingi  bilioni 20  kutokana na kuzushiwa kifo na kwamba fedha hiyo haitapungua hata shilingi mia.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni